...
Bidii Inalipa! | | | Kiswahili

Description: Vipaji vya Wanakokotoa! Fursa ya kusisimua, kushiriki katika
mashindano ya vipaji. Kibena, Kiduchu na Amani wamejiandaa
kucheza vilivyo…lakini wanahitaji mavazi maalum. Na kupata
mavazi hayo, wanahitaji kumlipa fundi cherehani. Na kumlipa
fundi cherehani, hela inahitajika…Watapataje hela na watajifunzaje
thamani ya hela katika mchakato huo?

Topic: Elimu ya Fedha: Kipato

Age Range: 7 – 14 years

Language: Kiswahili

Content Type: Video

...
Iambie Pesa pa Kwenda | | | Kiswahili

Description: Wanyama wa Kokotoa wanatambua umuhimu wa elimu.
Kwahiyo muda wowote, wanakaa chini ya mti na kujifunza.
Kiduchu na rafiki zake wanataka kuwasaidia kujenga darasa lakini
wana hela kidogo ya kufanya yote hayo. Vitu gani ni mahitaji na
vipi ni matakwa, na watapangaje bajeti yao?

Topic: Elimu ya Fedha: Kupanga Bajeti & Matumizi

Age Range: 7 – 14 years

Language: Kiswahili

Content Type: Video

...
Kwa Uzuri au Ubaya | | | Kiswahili

Description: Watoto wa Ubongo wanaweka taarifa zao binafsi kwenye mtandao.
Kwahiyo Mama Tech amejua vitu kadhaa kutoa kwao…kuna kitu
cha kujifunza hapo!

Topic: Teknolojia ya Mawasiliano

Age Range: 7 – 14 years

Language: Kiswahili

Content Type: Video

...
Tunachoweza Kula | | | Kiswahili

Description: Mama Koba amelazwa hospitali kwa ajili ya kisukari. Watoto wake
wapendwa, Koba na Baraka wanataka kumfanya ajisikie nafuu.
Kwahiyo wanampelekea chakula kitamu…chipsi zilizoongezwa
chumvi, soda, aisikrimu…na vingine ambavyo daktari ANAVIKATAA!

Topic: Lishe

Age Range: 7 – 14 years

Language: Kiswahili

Content Type: Video

...
Sisi ni Mfano wa Kuigwa | | | Kiswahili

Description: Baraka na Koba wanajifunza kuhusu kuwa mfano mzuri kwa mdogo wao Mwenda huku wakichunguza kuhusu manda nzima malezi ya awali ya watoto. Koba hakwenda shule na anahitaji kuazima daftari la Kibena ili aandike notsi lakini anakumbana na changamoto pale Mwenda anapoharibu daftari la Kibena! Wakati akijaribu kutatua changamoto hiyo, anaishia kujifunza kuhusu ukuaji wa ubongo kwa kupitia Mwenda kuliko ambavyo notsi za kwenye daftari zingemfundisha.

Topic: Maendeleo ya Awali ya Watoto: Ukuaji wa Ubongo

Age Range: 7 – 14 years

Language: Kiswahili

Content Type: Video

...
Kuwa Huru | | | Kiswahili

Description: Kiduchu anataka kufanya useremala. Koba anataka kupika.
Mwalimu Mlea anataka kila mtu afanye kazi kulingana na jinsia
yake. Kwani, haya mambo ya kufanya kazi kutokana na jinsia
yalianzia wapi? na nani alisema iwe hivyo? Kiduchu ana
msimamo wake!

Topic: Usawa wa Kijinsia

Age Range: 7 – 14 years

Language: Kiswahili

Content Type: Video

...
Niulize Kwanza! | | | Kiswahili

Description: Hakuna shaka kabisa kwamba Kiduchu ana mtindo wa nywele wa
kipekee Kokotoa nzima. Yeye anajua, na sisi tunajua hilo pia.
Lakini kuna watu ambao wanajaribu kuzirekebisha. Kiduchu
hataki nywele zake zirekebishwe na kutokana na hilo, yeye na
marafiki wa Ubongo wote wako kwenye safari ya kuelewa kuhusu
ridhaa na kutumia haki yao ya kutoa ridhaa kwa chochote kile
kinachofanyika kwao na katika miili yao.

Topic: Ridhaa

Age Range: 7 – 14 years

Language: Kiswahili

Content Type: Video

...
Kuwa Salama Wakati Wote | | | Kiswahili

Description: Ni siku ya mechi ya fainali za ligi ya mpira wa miguu iliyosubiriwa
sana. Kila mtu yuko kwenye TV akiangalia. Wakati mchezo
umekolea, ghafla…umeme unakatika! Ungana na watoto wa
Ubongo katika harakati zao za kurudisha umeme Kokotoa…
huku wakijifunza kuhusu sakiti na umeme!

Topic: Umeme/Sakiti

Age Range: 7 – 14 years

Language: Kiswahili

Content Type: Video

...
Uamuzi Mgumu | | | Kiswahili

Description: Kiduchu anataka kuwa na muda zaidi wa mazoezi ya mpira wa
miguu, lakini pia anatakiwa kurudi kufanya kazi za nyumbani.
Kazi za kaka yake, zinamruhusu kuwa nje ya nyumbani kwa
muda anaotaka. Amani anaingia matatizoni kwa kuchelewa
kuingia darasani kwasabbau vyoo vya wasichana viko mbali
sana. Timu ya mpira wa miguu ya Kokotoa inashindwa kuamua
kuhusu rangi yao mpya ya vifaa vya vya mpira wa miguu!
Inaweza kuonekana kama purukushani hivi, lakini ni fursa ya
kujadiliana ili kupata muafaka.

Topic: Ujuzi wa Kujadiliana na Kufikia Muafaka

Age Range: 7 – 14 years

Language: Kiswahili

Content Type: Video

...
Inyuguti A | Short Clip | Alphabet | Kinyarwanda

Description: Akili and her friends learn how to vocalize letter “A” and forming words by using letter “A”

Subject: Pre-Literacy

Age Range: 3 – 6 years

Language: Kinyarwanda

Content Type: Video

1 15 16 17 18 19 89